Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 348 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la Mlima shabaha kata ya Muungano wilayani Hai kupitia mradi wa kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Shule hiyo inatarajia kupunguza msongamano wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya kambi ya raha na Mlima shabaha zilizopo kata ya Muungano.
Akizungmza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanywa na kamati ya Fedha ,Uongozi na Mipango mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amemshukuru rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zitatatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.
Amesema ujenzi wa shule hiyo pia utasaidia wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sanyastation ambao ulazimika kuvuka mito wakati wa mvua.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi wilaya ya Hai Hussen Kitingi amesema ujenzi wa madarasa hayo unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023 na kwamba taratibu za awali zimeshafanyika.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai