Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga ameishukuru kampuni ya kambele Investment kwa msaada wa saruji na kompyuta ikiwa ni kwa lengo la kurudisha kwa jamii faida waliyopata.
Ameyasema hayo wakati akipokea msaada huo wa mifuko Mia moja ya siment pamoja na kompyuta kutoka kwenye Kampuni hiyo
Aidha ametoa wito kwa kampuni zingine na wafanyabiashara kuiga kutoka kwa kampuni ya kambele Investment kwani msaada huo wa siment utasaidia kwenye mahitaji mbalimbali kama ujenzi wa matundu ya choo kwa shule ambazo miundombinu yake haiko sawa
Pia ameitaka kampuni ya hiyo kufata kanuni katiba na miongozo ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuepuka migogoro ya kuuza maeneo mara mbili kwani wananchi wanapaswa kupata huduma bora hvyo nivyema kujitaftia kipato vya halali.
Nae Mkurugenzi wa Kambele Investment Winston Kambele amesema kuwa wametoa mchango huo ili kuunga mkono katika juhudi za kujenga wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai