Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amehamasisha wadau wa elimu mkoani Kilimanjaro kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wenye ulemavu.
Zoezi hilo limefanyika katika kongamano la wiki ya elimu lililofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Sintoo amesema kuwa anafurahi kuona watoto wenye ulemavu wakisaidiwa na kupata elimu kama watoto wengine kwa kuwa ni haki yao ya msingi na akawa mfano kuchangisha jambo lililowahamasisha wengine kujitolea kuchangisha
Pia Sintoo amewashukuru masista wa shule ya Mtakatifu Francinsi iliyopo Bomangombe wilayani Hai pamoja na Kanisa Katoliki kwa namna wanavojitolea kuwalea watoto hao kwa upendo na kuwasihi wadau mbalimbali kujitolea kuwahudumia kwa upendo.
Kwa upande wake sista anaewahudumia watoto hao wa shule ya Mtakatifu Francisi ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia misaada mbalimbali kama vile chakula na kuwa nafuu katika kuwahudumia watoto hao.
Sista huyo amesema fedha zilizopatikana atazitumia kununulia vitanda kwa ajili ya watoto hao na atampelekea taarifa ya mapato na matumizi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mgwhira na kuwashukuru wale wote waliochangisha fedha hizo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai