Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya kwa kubuni na kuboresha vyanzo vya mapato wilayani humo.
Dkt. Mghwira ametoa pongezi hizo alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na kusema kuwa halmashauri yeyote haiwezi kujiendesha pasipo kuwa na mapato.
Ametaja baadhi maeneo ambayo serikali wilayani hapo imeboresha ni pamoja na upatikanaji wa mapato katika eneo la utalii chemchemi ya maji moto maarufu kama (chemka) na stendi kuu ya mabasi Bomang’ombe.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mijongweni na kuwataka maafisa kilimo na mifugo wa wilaya kupiga kambi ya siku 15 kijijini hapo ili kuwaelimisha wananchi namna bora ya kulima kilimo chenye tija na ufugaji wa kisasa.
Naye mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ametoa onyo kwa serekali ya kijiji kutokugusa mali za wananchi huku akitaja kijiji hicho kuwa ni kati ya vijiji vilivyopokea fedha za miradi mikubwa ikiwemo kiasi cha shilingi milioni 200 kilichotolewa na shirika la Kijapani JIKA.
Awali akitoa taarifa ya halmashauri, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Jacob Muhumba amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa halmashauri ya Hai iko mstari wa mbele kutekeleza maagizo ya Mkoa na Serikali kwa ujumla katika kuwahudumia wananchi na kuwapunguzia kero.
Mkuu wa Mkoa huyo amefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambapo amezungumza na watumishi wa Umma na kuwakumbusha wajibu wao, amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mijongweni.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai