Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Amiri Mkalipa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaojaribu kudokoa kwa namna yoyote fedha zinazoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo.
Mhe. Mkalipa ametoa onyo hilo wakati akikabidhi mradi wa ujenzi wa chuo cha ufundi VETA wilaya ya Hai kwenye hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Elerai na kuwataka wananchi kuwa walinzi wa miradi kwenye maeneo yao.
"Mlinzi wa kwanza wa vifaa vya ujenzi wa miradi ni wewe mwananchi, ikiwa sasa tunaleta vifaa mnaiba inabidi tuwalete askari waje walinde saruji, hivi inawezekana? Wananchi- hapana, waambieni vijana wenu wenye tabia za wizi, mkuu wa wilaya amesema atatoa mfano kwa kijana atakayejaribu hata robo ya saruji au msumari mmoja, kila mzazi akamwambie mtoto wake vipo vya kuchezea lakini siyo mradi wa veta"
Aidha mkuu wa wilaya amemtaka mhandisi wa wilaya kuhakikisha wananchi wa eneo husika wanapata fursa ya ajira za ujenzi badala ya kuchukua vibarua kutoka nje ya eneo hilo hususan katika ujenzi wa chuo hicho ambao unatarajia kuanza mwezi huu wa saba 2023.
"Jambo la kuzingatia, diwani na viongozi wengine mhakikishe wana Elerai wanapata ajira, wale mafundi watakaopewa kazi angalia maslahi ya wana Elerai kwa maana ya watu watakaokuwa wanafanya vibarua wapate maslahi yao lakini wapate hizo kazi na kusiwe na urasimu kwenye jambo hilo"
Mdhibiti ubora wa Elimu wilaya ya Hai Asteria Kawau wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi, amewapongeza wananchi wa eneo la Elerai kwa kujitolea eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho cha VETA ambapo baada ya kukamilika kwa ujenzi huo kunatajwa kuwanufaisha vijana wengi wa wilaya ya Hai hususani
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai