Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya amelitaka Jeshi la akiba kwakushirikiana na jeshi la polisi kuanza mara moja opareshini za mara kwa mara zitakazo wezesha kujua maeneo yote yanayohusika na uuzaji wa madawa ya kulevya pamoja na utengenezaji wa pombe haramu aina gongo ndani ya wilaya.
Ametoa agizo hilo hii leo wakati wa kikao kazi na askari wa jeshi hilo la akiba katika viwanja vya Halmashauri hiyo ambapo amesema hivi sasa ni wajibu wao kuhakikisha wanafanya opereshini hiyo ambayo pia itasaidia kujua, kutambua wageni wote wanaoingia wilayani hapo na shughuli wanazozifanya kwa muongozo wa polisi kata lengo likiwa nikuhakikisha kuwa wilaya ya Hai inakuwa salama wakati wote.
Pia amewatahadharisha kutokumuonea mtu yoyote wakati wa opareshini hiyo huku akiwaasa kutokujiingiza katika biashara ya uuzaji wa madawa ya kulevya pamoja na pombe haramu na atakae bainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria na kinidhamu.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Hai Pendo Wela amewataka kuwa na uzalendo ,nidhamu na kuzingatia kiaopo walichokiapa ili kuwetekeleza majukumu yao kikamilifu.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Elia Machange amesema kuwa wao kama halmashauri wako tayari kushirikiana na jeshi hilo wakati wote huku akilipongeza kwani limekuwa na mchango mkubwa wakuchangia amani kwa wakati wote ndani ya wilaya.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai