Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Juma Irando amezindua vitabu vya Mkakati wa kuboresha Elimu nchini katika Halmashauri ya wilaya ya Hai huku akiwataka Walimu kuzingatia maadili ya kazi zao.
Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Septemba 16, 2022 wakati wa kikao Cha wadau wa Elimu wilayani Hai kilichofanyika kwenye Ukumbi wa chuo cha Ufundi Kilimanjaro Modern wilayani humo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulikwenda sambasamba na kugawa vitabu kwa Maafisa Elimu kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu, DC Irando ameeleza kuwa vitabu hivyo vitatumika kama mwongozo katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Tawala wilaya hiyo Upendo Wella ametoa rai kwa waalimu hao kuhakikisha wanaitumia miongozo hiyo ambayo imezinduliwa katika ngazi ya wilaya ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai David Lekei amewataka walimu kufanyakazi kwa kuzingatia miongozo ili kuendelea kudumisha rekodi nzuri ya Elimu ndani ya wilaya hiyo.
Naye mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari Julius Mduma ameeleza kuwa vitabu hivyo vitakuwa na kigezo cha kupima mwenendo wa ufundishaji kwa Shule za msingi na Sekondari.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai