Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Juma Irando amesema ameridhishwa na kasi ya Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa unaotekelezwa katika shule 7 wilayani humo kupitia nguvu kazi ya ndani (force account).
Shule hizo ni pamoja na shule ya Sekondari Longoi, shule ya Sekondari Rundugai, Hay day, Shule ya Sekondari Tumo, Neema Sekondari, Roo pamoja na shule ya Sekondari Mukwasa.
"Katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya Ujenzi wa madarasa, Irando akatoa rai kwa wananchi "miradi hii ni yetu wote, tunahitaji sana sapoti au nguvu za wananchi kwa ajili ya kuendeleza hii miradi"
"Na kimsingi nimeelekeza pale popote ambapo wananchi watafanya chochote, lazima nguvu zao zithaminishwe tuweze kujua michango yao kwa thamani ya fedha na lazima ifike sehemu tuwaambie ili waweze kujua kkwamba tumetambua kazi yao nzuri waliyofanya kuisapoti Serikali"
"Kwa watendaji, tuendelee kuifatilia miradi yetu kwani inatakiwa ikamilike kwa wakati ili kuepuka usumbufu kwa wanafunzi wetu mwakani, lakini pia thamani ya fedha lazima ionekane kwenye miradi pamoja na muda kwa maana ya wakati"
"Na wote tunajua kwamba mwakani mwezi wa kwanza wanafunzi wataanza kujiunga na kidato cha kwanza hatutegemei upungufu wa madarasa uendelee kuwepo na ndiyo maana tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliona hilo na akatoa fedha nchi nzima, sasa wananchi wetu wa Hai lazima tushirikiane na mama"
Aidha Irando amewaagiza wakuu wa shule kujiunga kwa pamoja na kuona namna nzuri ya kuagiza vifaa vya Ujenzi kwa lengo la kupata unafuu kwenye bei na kuokoa baadhi ya gharama
Naye Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Hai Josiah Gunda ameonya wale wote wanaosimamia miradi hiyo kutokuthubutu kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye fedha za miradi hiyo kwani taasisi hiyo iko macho wakati wote.
Wilaya ya Hai ilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 200 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, ambapo kila darasa moja linagharimu jumla ya shilingi milioni 20
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai