Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuisimamia miradi ya maendeleo iliyopo kwenye kata zao na kuhakikisha inamalizika kwa wakati na kwa ubora.
Hayo yamesemwa leo Julai 28, 2022 na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka kwenye baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Rutaraka amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya asilimia 94 ya mapato kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 kwa mwaka wa fedha uliopita ambapo waliweza kukusanya asilimia 82.
Akizungumza katika kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amewapongeza madiwani kwa utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Aidha mbunge huyo amemtaka Meneja wa Tanesco wilaya ya Hai kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu na viongozi wa mradi wa maji Bomang’ombe – Kikafu soka ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai