Jamii imetakiwa kushiriki kikamilifu katika suala la malezi kwa mtoto ili kuondokana na changamoto ya malezi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ndugu Japhet Mselle amesema kuwa jamii inatakiwa kuonya watoto juu ya tabia hatarishi ikiwa na pamoja na kuweka mbali tamaduni zilizoletwa na wakoloni na kudumisha tamaduni halisi za jamii husika.
Mselle ambaye pia chifu Ameeleza kuwa watoto wanapata malezi katika sehemu kuu tatu ikiwa ni kwenye nyumba za ibada shuleni na nyumbani na kusema kuwa maeneo haya matatu yasipokuwa salama jamii itaharibu kabisa watoto, kwani kipande cha jamii katika malezi ya mtoto kimekosa nguvu.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuangalia mambo ya msingi kama yaliyokuwepo awali kama kuwaonya watoto na vijana kupitia wazee ili wapate maadili mazuri kwani watoto ndio taifa la kesho.
Pamoja na hayo, ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa wawafundishe watoto maadili bora, kwani nyumba za ibada na shule hazitoshi kuwaelekeza namna bora ya kuishi katika jamii inayowazunguka.
Kwa uapande wake Afisa Ustawi wa Jamii halamsahauri ya wilaya ya Hai Helga Simon amesema
Kwa upande wake Mchungaji Emily Hayishi amewataka wazazi kutimiza wajibu wao katika malezi ya familia na hasa kusimamia maadali ya watoto ambao kwa hivi karibuni yanadaiwa kuporomoka, amesema wazazi wengi wameacha jukumu la malezi kwa wasichana wa kazi.
“hali ya watoto wetu ni mbaya kuliko tunavyofikiri kutokana na aina ya maisha tunayoishi,malezi tumewaachia wasichana wa kazi ambao hatujui malezi yao yalikuwaje,yawezekana walilelewa katika mazingira na maadili yasio faa na tunategemea kuwa na kizazi chenye maadili bora?”aliuliza Mchungaji Hayishi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai