Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira amezitaka taasisi na mashirika kushiriki katika aina mbalimbali za uwekezaji ikiwemo kwenye sekta ya fedha kupitia dhamana za serikali.
Dkt. Mghwira ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo kuhusu aina za dhamana za serikali yenye lengo la kutoa elimu kwa wadau kushiriki kwenye aina mbalimbali za uwekezaji
"Dhumuni la mafunzo haya ni kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya dhamana za serikali pamoja na kuanzishwa kwake, jambo pili ni faida za dhamana za serikali kwa wananchi ambao wanataka kuwekeza kwenye sekta ya fedha kwa dhamana za serikali" amesema Dkt Mghwira.
Kwa upande wake kaimu meneja wa fedha na uendeshaji kutoka Benki kuu ya Tanzania kanda ya Arusha Bw. Haruna Shamte amewataka wadau na viongozi walioshiriki kwenye mafunzo hayo kuifikisha elimu hiyo kikamilifu kwa wawekezaji.
"Mwaka jana tumetoa elimu katika mkoa wa Tanga na mwaka huu tuko hapa Kilimanjaro lengo ni kuhakikisha kuwa tunawafikia wadau mahali ambapo wapo hivyo viongozi waliopata elimu waifikishe kwa wale watu ambao wako chini yao" amesema Shamte.
Naye mwenyekiti wa halmshari ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka ambaye ameshiriki mafunzo hayo amebainisha kuwa ni wakati sasa wa kwenda kuzungumza na wawekezaji katika wilaya hiyo juu ya umuhimu na faida ya uwekezaji wa fedha kupitia dhamana za serikali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai