Ushirikiano kati ya Mamlaka wa usambazaji Maji na Usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) , WAKALA wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Hai utasaidia kuharakisha miradi inayotekelezwa na Serikali katika kukamilika kwa wakati kwenye maeneo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai , Edmund Rutaraka ameyasema hayo wakati akifunga kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichojadili rasimu ya bajeti RUWASA na TARURA kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya shughuli zinazotarajiwa kufanyika kwa msimu huo.
“Mkiwa mnaandaa hizi bajeti au kuna kitu mnataka kufanya mtushirikishe ili tuweze kwenda pamoja,kwahiyo nawapongeza sana TARURA na RUWASA kwa taarifa zenu mlizozitoa hapa naamini tutakwenda kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunatimiza yale malengo tuliyoyaweka kila mwaka”amesema Rutaraka
Naye mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Irando aliwata wataalamu wa TARURA na RUWASA kufanyakazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa wanasimamia miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma bora zilizokusudiwa kuwafikia
Irando amesema serikali imekusudia kuboresha huduma zote muhimu ikiwemo maji na barabari ili kuwaondolea kero wananchi wanazokutanazo hususani kuimarisha ubovu wa miundombinu ya barabara kutokana na baadhi kutokupitika kwa msimu mzima wa mwaka.
“Barabara zote ambazo hazijasajiliwa zifunguke na kama kuna hela ambayo inatakiwa itengwe kwa ajili ya mapato ya ndani hilo pia lifanyike” amesisitiza DC Irando
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai