Serikali imesema itajenga mahakama mpya ya mwanzo ya machame baada ya ile ya zamani kuchakaa.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe likiuliza ni lini serikali itapeleka hakimu ili mahakama hiyo ianze kutoa huduma za kimahakama.
Gekul amesema licha ya jengo liliopo kukarabatiwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo pamoja na wadau wa maendeleo, lakini serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mahakama mpya kwakuwa mahakama iliyopo ni kongwe.
Naibu Waziri wa katiba na sheria amemshukuru mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe kwa kutoa fedha za kukarabati jengo hilo la mahakama ya mwanzo.
“Nimpongeze Sana Mhe. Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe kwa moyo wakujitolea kufanya ukarabati wa jengo hilo la mahakama lakini katika jengo lile bado lina ‘crack’ yingi (nyufa) ndio maana serikali imeweka mikakati yakujenga jengo jingine la mahakama ya mwanzo katika Kata ya machame ":Gekul
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 27 Hai
Simu: 0272758441
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai