Serikali imesema kuwa inatekeleza mpango wa malezi na makuzi ya watoto wa kike na wa kiume kwenye umri wa awali ambapo hiyo inakwenda sambamba na ujenzi wa kulea watoto hao kwenye ngazi ya jamii.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wananwake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe aliyetaka kujua kuwa Serikali ina mpango gani wa kumjengea uwezo mtoto wa kiume ili kuja kuwa baba Bora hapo baadaye.
"ni kweli kabisa tunatambua sasa hivi watoto wa kiume wanakumbwa na changamoto nyingi sana tofauti na awali zitokanazo na mmomonyoko wa maadili na kukosa malezi na makuzi bora kiasi kwamba hata akiwa baba atashindwa kuwa baba mzuri na kupambana na changamoto za familia. katika hili serekali inatekeleza mpango wa malezi na makuzi ya watoto kwenye umri wa awali ambapo hii inaenda sambamba na ujenzi wa vituo vya kulea watoto hawa kwenye ngazi ya jamii na huko tutakuwa na watoto wa kike na kiume."
Akieleza kuhusu mpango wa pili amesema utahusu kuwawezesha vijana wenye umri wa kuelekea huku akielezea kuwa mpango huo utakuwa utakuwa na mwongozo mzuri utakao mwezesha kijana wa kiume kujua changamoto atakazo kutana nazo atakapofikia hatua ya kuitwa baba.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai