Serikali katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imeelza kuridhishwa na utendaji kazi wa jeshi la polisi wilayani hapo.
Akizungumza na maafisa na askari wa jeshi hilo pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa jeshi hilo, mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amesema kuwa jeshi hilo limekuwa likitekeleza vizuri majukumu yake kwa utendaji bora na wakuigwa kutokana na kufuata misingi na taratibu za ulinzi na usalama.
Amesema kuwa jeshi hilo limefanya kazi mbalimbali zikiwemo kuu tatu ambazo zimeipa sifa kwa ukamataji na uandaaji wa mashtaka kwa watuhumiwa waliojihusha na kuzambaza noti bandia, wizi wa mifugo pamoja na kudhibiti kiwanda cha kutengeneza pombe bandia sina ya konyagi.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa jeshi hilo la polisi ambavyo ni pamoja na saruji mifuko 100 tofali elfu mbili, mchanga tani 21 na tairi 8,Sabaya amesema kuwa Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais Magufuli yanawataka wasaidizi wake kuhakikisha vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo yao wanayoyaongoza vinafanya Kazi katika Mazingira mazuri yatakayowawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa uwaminifu.
Aidha amelitaka jeshi la polisi wilayani Hai kuongeza juhudi katika kutekeleza majukumu yao hasa katika kupambana na wahalifu wa aina mbalimbali kwa mujibu wa sheria na kuepuka kufanya uonevu kwa Ria wasiokuwa na hatia
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa Leo ni kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa jeshi hilo la polisi wilayani Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai