Katibu tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wella ametoa siku 3 kwa wafugaji waliovamia kijiji cha Kimashuku kata ya Mnadani wilayani humo kuondoka na mifugo yao katika kijiji hicho.
Ametoa maagizo hayo katika mkutano na jamii za wafugaji na wakulima uliofanyika katika ofisi ya kijiji hicho na kuhusisha kamati ya ulinzi na usalama wilaya, viongozi wa kata, wataalamu mbalimbali na viongozi wa kijiji hicho.
Katibu tawala huyo ameeleza kuwa maamuzi hayo yamekuja kufuatia mkutano wa kuwasikiliza wananchi wa jamii zote mbili za wakulima na wafugaji na kusema kuwa wamesikiliza na busara ni kuwa wafugaji waliovamia kijiji hicho kinyume na sheria na kuwa waondoe mifugo yao kuepusha vurugu na migogoro inayoweza kuepukika.
Akitolea ufafanuzi wa kisheria kuhusu kuhamisha mifugo kaimu afisa mifugo wilaya ya Hai ndugu David Saba amesema ili kuhamisha mifugo kutoka kijiji kimoja kwenda kingine lazima apate kibali kutoka kwa ofisi ya mkuu wa wilaya sambamba na vibali kutoka kwa vijiji vyote viwili anakotoa na anakopeleka mifugo.
Kwa upande wao wananchi wameshukuru viongozi hao kufika katika kijiji chao na kutatua kero hiyo ambayo inatajwa kusababisha ukosefu wa amani na njaa kijijini hapo.
Wella amesema atakae kaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na kuwataka wanachi kuwawavumilivu na kutokuchukua sheria mkononi ili kuepusha madhara yatokanayo na vurugu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai