ZOEZI la uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro limekamilika katika hali ya utulivu na amani huku wananchi wakijitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi wao.
Uchaguzi huo umefanyika Novemba 24 mwaka huu, umehusisha viongozi wa nafasi za wenyekiti wa vijiji, vitongoji na wajumbe wa halmashauri kupitia makundi ya wanawake na kundi mchanganyiko.
Akizungumzia uchaguzi huo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo , Juma Masatu amesema kuwa uchaguzi huo umemalizika salama na wananchi wametumia haki yao ya msingi kuwapata viongozi watakaosimamia shughuli zote za kimaendeleo .
“Uchaguzi huu hufanyika chini ya Ibara ya 8 (1) (a) ya Katiba ya Tanzania kuwa ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii na kuwa ndiyo msingi wa mamlaka yote iliyonayo serikali hupata kutoka kwa wananchi.”amesema Masatu
Jumla ya wenyeti wa vijiji 62, na wenyeviti 294 wa vitongoji wamepatikana kuongoza nafasi kwa kipindi cha miaka mitano hadi hapo mwaka 2024 utakapofanyika uchaguzi mwingine.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai