Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Mhe. Edmund Rutaraka amesema Halmashauri ya wilaya ya Hai imefanikiwa kuvuka lengo la kukusanya mapato kutokana na ushirikiano ulipo kati ya viongozi wa Wilaya hiyo.
Rutaraka ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani robo ya nne kilichofanika leo 01/08/2024 katika ukumbi wa Halmashauri na kuongeza kuwa Halmashauri hiyo imekusanya zaidi ya asilimia 100 ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amsema halmashauri iliweka lengo la kukusanya bilioni 4.2 lakini hadi mwaka wa fedha unaisha wamefanikiwa kukusanya bilioni 4.5 na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fedha za miradi ya maendeleo zinazotokana na mapato ya ndani. (40% kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutoka kwenye mapato ya ndani)
Aidha ametoaa shukrani na pongezi kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Maafue kwa kupeleka changamoto na kufatilia fedha hizo.
Pia ametoa pongezi kwa madiwani, kamati ya Ulinzi na Usalma wilaya ya Hai, Pamoja na watumishi kwa ushirikiano wanaoneshaa na kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dionis Myinga amesema Halmashauri hiyo imepokea fedha za utekelezaji wa miradi mingi na mingine ikiwa ni nje ya bajeti.
“Tumepokea fedha bilioni 10.6 kwa ajili ya miradi, sasa tuna deni kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na deni hili ni kufanya kwa bidi na kuendelea kusimamia miradi kikamilifu” amesema Myinga.
Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa Zahanati ,Vituo vya Afya, Shule na ongezeko la madarasa katika shule za Sekondari na Msingi Wilayani humo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai