Vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vinavyotarajiwa kupokea mkopo usio na riba hivi karibuni unaotokana na asilimi kumi za mapato ya ndani ya hamashauri wametakiwa kuzingatia andiko lililowawezesha kupata mkopo.
Akizungumza katika warsha ya mafunzo ya ujasiriamali yalioandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii kwa vikundi hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo David Lekei amewasisitizia wajasiriamali hao kuzingatia andiko la mradi kwakuwa ndio dira ya uendeshaji wa huduma au biashara wanazoenda kufanya.
“ukiona umefika hapa ina maana kuna vigezo umekidhi, ikiwa ni pamoja na andiko la mradi, hivyo ni vema mkafanya biashara kwa kufuata andiko,msiende kubadili matumizi ya fedha hizi jambo linaloweza kuwasababisha adha kubwa wakati wa kurejesha”.
“mafunzo yanatolewa ili hizi fedha mkazitumie kwa kufuata kanuni na taratibu, mzingatie sana mafunzo haya hapa tuna mtu wa TAKUKURU ,tuna Mtu wa usalama barabarani ili kuwapitisha katika mambo yote ya msingi ”.alisisitiza Lekei.
Naye Mkuu wa Divisheni ya maendeleo wilayani Hai Robert Mwanga amevitaka vikundi hivyo kufanya vizuri katika kazi wanazoenda kufanya ili lengo la serikali la kuboresha uchumi wa makundi hayo litime.
“Lengo la serikali ni kumuinua mwananchi kiuchumi, kukopesha na kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara sio kufikishana mahakamani hivyo kwa vile vikundi ambavyo vilipata mikopo katika awamu zilizopita zilipe mikopo hiyo kwa mujibu wa sheria kuepuka kufikishana mahakamani”alisisitiza Mwanga
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai