VIONGOZI waliochaguliwa kwenye Ucchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 wametakiwa kuwahudumia wananchi bila ubaguzi na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani ndiyo chanzo cha migogoro.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya mara baada ya zoezi la kuwaapisha viongozi hao wa mitaa lililofanyika kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Sabaya amesema kuwa viongozi wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa wakitoa haki bila ya ubaguzi itasaidia kutimiza ndoto za wananchi waliowachagua za kuwaletea maendeleo na wao kuishi bila migogoro.
Amesema viongozi waliochaguliwa ni vema wakatanguliza maslahi ya waliowachagua na kutimiza matarajio yao ili wazidi kupata maendeleo, huku akiwataka kwenda kusimamia kikamilifu ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakae kiuka sheria bila na kuhakikisha kuwa hawamuonei mtu.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Hai Juma Masatu amewataka viongozi walioapishwa kwenda kusimamia maendeleo katika maeneo yao na kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaenda kuleta faida kwa wananchi wakizingatia sheria na kuwakumbusha kuwa cheo walichokipata ni dhamana.
Uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika kote nchini Novemba 24 mwaka huu ambapo wilayani Hai Chama cha Mapinduzi kilifanikiwa kupata ushindi katika vijiji vyote 62, vitongoji na halmashauri za vijiji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai