Rai imetolewa kwa Viongozi wa dini wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kuongoza katika kuombea uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa leo na Katibu tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wella katika kikao kilichowakutanisha wadau wa uchaguzi huo pamoja na msimamizi wa jimbo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, kikiwa na lengo la kutoa maelekezo mbalimbali yanayohusu uchaguzi huo.
Amesema kuwa ni vyema sasa viongozi wa kisiasa na wakidini wakashirikiana katika kuwaandaa wananchi katika kuelekea uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kuhimiza zaidi amani na umuhimu wa kuwachagua viongozi hao kwani ni haki ya kila Rai.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi huo jimbo la Hai Bw. Juma Masatu amewataka watakao pata nafasi ya kuchaguliwa kuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuwa waadilifu na waaminifu pindi watakapokuwa wanasimamia uchaguzi huo ili kwenda na taratibu na sheria zilizowekwa.
Amesema ili zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa liweze kukamilika vizuri na kuweza kufanikiwa inawapasa wasimamizi wasidizi kuwa makini na kufuata kanuni na sheria zilizowekwa za uchaguzi kwa kuzingatia uadilifu na uaminifu.
Uchaguzi huo wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu nchini kote huku ukisimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa [TAMISEMI]
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai