Kamati za ulinzi na usalama za vijiji na kata zimetakiwa kushirikisha wananchi wa jamii zote na makundi yote katika kupanga na kufanya maamuzi yanayowahusu ikiwemo ikiwemo hali ya uhalifu inavyoendelea pamoja na utatuzi wake katika maeneo husika.
Kamishna msaidizi mwandamizi mstaafu Englibert Kiondo ameyasema hayo alipozungumza na viongozi wa vijiji, vitongoji na kata katika ukumbi wa KKKT wilayani Hai na kuwataka viongozi hao kwenda kukaa katika mikutano ya vijiji na kushirikisha wananchi kuhusu ya ulinzi na usalama.
"Mnatakiwa mkakae kwenye mikutano ya vijiji muwashirikishe wananchi kuhusu hali ya uhalifu inavyoendelea pale, ipigwe kura ya siri kwamba ni wanani wanatusumbua hapa, kamati ya usalama ya kijiji inakaa na Polisi kata wenu mnajadili yanapelekwa ngazi ya kata yanachujwa pale yanaletwa ngazi ya juu, Mtendaji kata yupo, DC yupo watachambua watachambua changamoto za kila kata"
"Tumesema tuunde vikundi vya ulinzi shirikishi Polisi kata ameshindwa kuunda kwa sababu vijana wote ni walevi, badala ya kwenda kulinda wanapaka nyumba alama za kuja kuvunja usiku na mwenye jukumu la kusema walinzi shirikishi ni watu gani, ni Mwenyekiti wa kijiji na kamati ya ulinzi na usalama" ameongeza Kamishna Kiondo
Kaimu mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Hai David Lekei akizungumza wakati akiahirisha mafunzo hayo amewataka wenyeviti wa vijiji, watendajj wa vijiji na kata kusimama kwenye nafasi zao kwa kutatua changamoto zilizopo kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuonyesha hatua walizochukua kukabili changamoto hizo.
Awali mhadhiri wa chuo cha usimamizi wa mahakama (IJA) Lushoto, Kelvin Mandopi wakati akitoa mada kwenye kikao hicho cha mafunzo amewataka viongozi wa vijiji, vitongoja na kata kwenda kushauri masuala ya kiulizi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuweka misingi mizuri ya kukomesha uhalifu.
Naye mhadhiri kutoka idara ya sayansi ya siasa chuo kikuu cha Dar es Salaam Elijah Kondi akizungumzia umuhimu wa viongozi kwa polisi katika kufanikisha polisi jamii amesema kutatua mazingira ya kiuchumi na kijamii ndiyo suluhisho la uhalifu kutokea kwenye jamii.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Hai mrakibu mwandamizi wa Polisi Juma Majatta ametaka viongozi kuendelea kufanya kazi licha ya kuwepo tatizo la kisheria linapokuja suala la uhalifu "msivunjike mioyo tuendelee kutenda yale ambayo tunaamini yanaweza yakatusaidia kuondoa au kupunguza matukio ya uhalifu katika wilaya yetu ya Hai"
Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho cha mafunzo ni pamoja na Katibu Tawala wilaya ya Hai Upendo Wella, kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa, pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya hiyo Mrakibu msaidizi wa polisi Novatus Akondowe.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai