Katibu tawala wa wilaya ya Hai Sospeter Magonela amewataka wadau wa maendeleo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha watoto wenye umri wa mika 0-8 ndani ya wilaya wanapata huduma ya malezi jumuishi ili wastawi na kufikia hatua za ukuaji timilifu.
Magonela ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ambapo amesema twakimu zinaonyesha kuwa aslimia ishirini ya watoto chini ya miaka 5 wana udumavu.
Amesema watoto wakiwa na udumavu wanaweza kusababisha taifa kukosa watu wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa tija na hivyo kuathiri ukuaji wa uchumi.
Ili kukabilina na tatizo hilo amesema ni vema uwekezaji ukafanyika katika maeneo matano ya mfumo wa malezi jumuishi ambayo ni afya bora, lishe, malezi yenye mwitikio, fursa za ujifunzaji wa awali pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto.
Akitoa mada katika uzinduzi huo Mratibu wa Afya na Uzazi hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Hai Godfrey Ngaya amewataka amesema watoto wengi hawafikiiukuaji timilifu kutokana na kupata lishe duni,kunyimwa fursa za kucheza,ukatili,Msongo wa mawazo wa familia,msongo wa mawazo wakati wa ujauzito,kukosa chanjo pamoja na utapiamlo.
Amewata wazazi kuhakikiasha watoto wanapata lishe bora na kuwapa muda wa kucheza,maji safi pamoja na vifaa vya mtoto kuchezea ambavyo ufanya mtoto kuchangamsha ubongo wake.
“ni wangapi hapa wanawanunulia watoto wao vifaa vya kuchezea?, najua wengi wetu tunawanunulia watoto vitu vya kuchezea tena wengine si ajabu jana walinunua lakini hatununuzi vitu ambavyo vinamchangamsha mtoto,acheni kununua vitu vilivyo tayari kama mpira,garai au mdoli badala yake mnunulie mtoto vitu ambavyo akiunga unga anapata mpira,gari au mdoli hapoa utakuwa unachangamsha ubongo wa mtoto”alisisitiza Ngaya.
Naye Shekhe Ibrahimu Hamadi akichangia mada katika hafla hiyo ameishukuru serikali kuja na mrogramu hiyo jumiushi ya taifa ya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto wilaya ya Hai na kuitakata jamii kushirikiana katika malezi kwakua sula hilo sio la mtu mmoja.
“Suala la malezi sio la mtu mmoja,ni la jamii yote na lazima jamii ijifunze juu ya malezi bora kwakuwa watoto wanaharibika katika mazingira mbalimbali.aliongeza Shekhe Hamadi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai