Wafanyabiashara wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamekumbushwa kutumia mifumo ya kielektroniki kwa ajili kupata leseni ya biashara na kulipa mapato mbali mbali ya serikali kama wanavyotakiwa.
Akizungumza katika katika kikao cha Baraza la Wafanyabishara wa wilayani Hai Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Amir Mkalipa amesema serikli imeweka mifumo hiyo ili kuokoa muda wa walipak kodi pamoja na kuhakikisha kuwa mapato husika yanaaingia moja kwa moja kwenye mamlaka husika.
Mkalipa amewataka wale wote watakaokutana na changamoto yoyote wakati wa kukata leseni kwenye mfumo huo kufika katika ofisi za biashara kwa ajili ya kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake Afisa Biashara Wilaya ya Hai Velda Lyimo amewataka wafanya biashara waliofanikiwa kupata leseni kupitia mfumo wa TAUSI kuwa mabalozi kwa wengine.
Naye Afisa Msimamizi wa kodi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) mkoa wa Kilimanjaro Bw. Hadipoi Papa amesema makampuni yote ya biashara wanatakiwa kulipa kodi na kutoa risiti za kieletroniki kwa wateja na kwamba wafanyabiashara wasiolipa kodi watapewa adhabu kulingana na makosa watakayo kutwa nayo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai