Zaidi ya wakazi 3000 wa wilaya ya Hai wanatarajiwa kunifaika na ajira kupitia mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha uchakatajia wa zao la Parachichi kinachotarajiwa kujengwa wilayani Hapo.
Hayo yameelezwa na mbunge wa jimbo hilo Saashisha Mafue katika mahojiano maalum na kituo cha redio boma Hai fm .
Mh! Saashisha ameeleza kuwa toka alipoomba ridhaa ya kuliongoza jimbo la hai ndoto yake ilikuwa kulifanya wilaya ya Hai kuwa Hai ya kilimo na viwanda hivyo anafanya kazi kwa nguvu zake zote kuakikikisha hilo linatimia.
“Jambo ambalo ni uhitaji kwetu sisi ni Hai ya kilimo na viwanda ilituweze kupata kiwanda tumeshirikiana na wenzetu wa Taaf na waziri wa kilimo na mifugo Husen Bashe tumepata mdau alieonesha nia ya kujenga kiwanda hapa kwetu Hai na kitakuwa kiwanda kikubwa cha kipekee Africa mashariki cha kuchakata zao la prachichi na bidhaa mbali mbali zinazotakana na zao hilo”
Amesema kuwa hatua iliyopo kwa sasa ni mchakato wa kufata matakwa ya kisheria kwa mkutano mkuu wa bodi ya ushirika kukaa kwa kufuata taratibu za vyama vya ushirika ili waweze kutolea maamuzi na baraka.
“Mwekezaji huyu yuko tayari muda wowote kuaza ujenzi wa kiwanda hicho lakini pia nimshikuru sana mweshimiwa rais Samia Suluhu Hasan kwanamna ambavyo sasa wizara ya kilimo imebadilika sasa haionekani kilimo ni adhabu kwa sasa kilimo ni tija na watu wanahamasika kulima na kuwekaza katika kilimo.
Aidha mbunge huyo pia ameeleza kuwa ameshatembelea masoko makubwa na uuzaji wa bidhaa za kilimo katika nchi tofauti tofauti afrika na nje ya bara hili na kujiridhisha kuwa mazao ya wakazi wa hai yanaweza kuuzwa katika maeneo hayo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai