Wanachama wa Chama cha Akiba na mikopo cha Hai Teachers Saccoss wametakiwa kutambua kuwa wajibu wao mkubwa kwa chama hicho ni kuhakikisha kuwa wanaweka akiba ya kutosha ili kusaidia kujikwamua kiuchumia pamoja na kukisaidia chama hicho kusonga mbele.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa wanachama wa chama hicho, mkufunzi wa katika semina hiyo amesema kuwa jukumu kubwa la mwanachama ni kuhakikisha kuwa anajikita zaidi kwenye uwekaji wa akiba ambazo zitatumika kwa manufaa yao ya baadae.
"Tuwe na tabia ya kuweka akiba zaidi, tuache kuweka zile akiba za kisheria tulizozoea na badala yake tuweke kulingana na kiwango cha kipato ninachopata". Alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama hicho Baraka Owenya amesema kuwa mafunzo hayo ya wanachama yana lengo la kuwakumbusha kuhusu wajibu wao kama wanachama pamoja na wajibu wao katika kukiendesha chama badala ya kukopa pasipo kuweka huku pia akisema kuwa ni takwa la kisheria.
" kwa leo zaidi ya 80% wamehudhuria mafunzo haya na wote tumeshuhudia wakishiriki kikamilifu". Alisema Owenya
Hata hivyo amepongeza jitihada za wanachama wa chama hicho kwa kuwa chama hicho kinaonekana kukua siku hadi siku huku pia idadi ya wanachama ikiongezeka.
Naye Meneja wa Hai Rural Teachers Saccoss Bi. Beatrice Msuya amesema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwasaidia wanachama kuhusiana na huduma zinazotolewa na chama ikiwemo kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati.
"Kwetu sisi umuhimu wa semina hii ni kuwaeleza huduma zitolewazo na chama na jinsi ya kuzitumia huduma hizo ikiwa ni kwa faida endelevu, na niseme tu hadi sasa tunao wanachama hai zaidi ya 800 na utakumbuka awali tulikuwa na lengo la kupata wanachama hai 50 kwa mwaka jambo ambalo tumevuka lengo hadi sasa". Alisema Bi. Beatrice
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai