Wizara ya Fedha kupitia kitengo cha elimu wametoa mafunzo ya huduma za kifedha vijijini (CMG) ambapo mafunzo hayo yametolewa kwa zaidi ya siku 10 katika mkoa wa Kilimanjaro, mafunzo yaliyolenga kuwapa Wananchi wa Hai ni namna ya kuhifadhi na kutumia Fedha pamoja na kuwaasa kuwekeza katika sehemu zilizo sahihi.
Akizungumza Afisa Mwandamizi wa wizara ya Fedha Ndg.Salumu Kimaro amesema mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu kwa umma kuhusu mikopo na namna nzuri ya kuwekeza kwa faida, vilevile ametoa tathmini ya mafunzo na mafanikio makubwa waliyopata tangu wameanza kutoa elimu katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo zaidi ya watu Elfu 6 wamefikiwa na kupatiwa elimu ya Fedha.
Afisa maendeleo wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi.Pili Bayo ameishukuru timu ya mafunzo ya Fedha na ametoa faida za elimu hiyo kuwa yameleta chachu ya maendeleo kwa Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Nao Wananchi waliohudhuria mafunzo ya Elimu ya Fedha wameshukuru sana ujio wa Elimu hiyo kwa umma kwasababu imewapa uelewa mpana zaidi kuhusu namna ya kuendesha vikundi vilivyosajiliwa na matumizi sahihi katika Fedha wanazowekeza.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai