Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe ameiomba serikali kupitia Waziri wa ujenzi na uchukuzi kutengeneza daraja lililokuwa likitumiwa na wananchi hao linalounganisha kata ya Weruweru na kata ya Mnadani kutokana na daraja hilo kusombwa na mafuriko msimu wa mvua uliopita .
Maombi hayo yamekuja baada ya wananchi wa Kata hiyo kumweleza Mbunge kuwa wanapita juu ya kivuko cha treni baada ya daraja lililokuwa likiunganisha kata hizo kusombwa na mafuriko.
Saashisha amesema kuwa daraja hilo la Kata ya Weruweru ambalo lipo Kijiji cha kikavu chini lilikua daraja tegemezi kwa wananchi wa eneo hilo lakini baada ya mafuriko hayo wananchi wamekosa mawasiliano ya daraja inayowasaidia kufikia huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu.
"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani imedhamiria kuzuia vifo vya Mama na mtoto lakini kutokana na ukosefu wa daraja hili , baadhi ya wakina Mama wanajifungulia katika kivuko hicho cha reli na wakati mwingine watoto kupoteza maisha hivyo ni wakati wa serikali kuangalia kwa jicho la pekee namna ya kurejesha daraja hilo kwa haraka." alisema Mafuwe.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Weruweru Abdala Chiwili amemshukuru Mbunge kwa kufika katika eneo hilo na kujionea hali halisi na kusema kuwa daraja hilo ni kilio kutokana na umuhimu wake kwani kivuko cha reli wanachotumia ni hatari kwa maisha yao kwani treni inapita mara kwa mara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai