Serikali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imewataka wananchi kuhakikisha kuwa inaboresha mazingira kwa kupanda miti na kuitunza ili iweze kukuwa hali ambayo itasaidia kukabiliana na hali ya Ukame.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Amiri Mkalipa alitoa agizo kwa nyakati tofauti katika zoezi la upandaji kwa ajili maadhimisho ya wiki ya Muungano ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kiwilaya kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi, kupanda miti pamoja na michezo.
"Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mazingira yanaboreshwa kwa kupanda miti ,kuitunza na ninyi wananchi hakikisheni kwenye maeneo yenu mnapanda miti ya aina tofauti ikiwemo ya matunda ambayo itasaidia kutunza mazingira pamoja kupata matunda"
"Leo tumepanda miti kwenye maeneo ya Kia, Shule ya Sekondari ya wavulana Lyamungo na Shule ya wasichana Machame ,niwatake wananchi na viongozi mliopo kwenye maeneo husika kuhakikisha kuwa miti hii inalindwa na kukuwa na kuwachukulia hatua kwa mtu yeyote atakayefanya uharibifu kwenye miti hii"
Hata hivyo, Mkalipa aliwataka viongozi na wananchi kuacha tabia kuotesha miti kwa ajili ya kipindi cha matukio na badala yake watumie msimu wa mvua kupanda miti kwa wingi kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
Awali akitoa taarifa za uoteshaji wa miti,afisa misitu wa Wilaya, Mbayani Mollel amesema kuwa wamekusudia kupanda miti milioni moja na laki tano kwenye maeneo ya wazi pamoja na kwenye taasisi za Serikali na zisizo za Serikali.
|
|
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai