Kufuatia mvua za elnino zinazotarajia kunyesha hivi karibuni,zilizotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA mkuu wa wilaya ya Hai mheshimiwa Amir Mkalipa amewataka wananchi wa wilaya ya Hai kuchukua tahadhari ili kuweza kukabiliana na athari zinazoweza kutokea kutokana na mvua hizo.
Amebainisha hayo lipokuwa akizungumza na kamati mbalimbali za za maafa wilaya ya Hai katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai.
Amesema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa anachukua tahadhari kabla mvua hizo hazijaanza kunyesha ambapo pia amezitaka kamati za maafa za wilaya kuhakikisha zinatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza kama vile mafuriko.
Ameongeza kuwa kamati za maafa kuanzia ngazi ya kijiji zinatakiwa kujikita katika kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari za kujijkinga na maafa ikiwa ni pamoja na kuhama katika maeneo ya mabondeni.
Hata hivyo mkuu wa wilaya amewataka viongozi wa dini kufanya maombi na dua ili mvua hizi zinazotarajiwa kunyesha zisilete madhara makubwa kwa Taifa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai