Diwani wa Kata ya Masama Kusini mhe. Cedrick Pangani ,ametoa wito kwa jamii koundoa miti iliyopo pembezoni mwa barabara ya Mungushi Nkwamakuu ili kupisha ujenzi wa barabara katika eneo hilo.
Ameyazungumza hayo katika kipindi cha siku mpya kinachorushwa na redio boma Hai fm mapema hii leo.
Pangani amesema Tarura wapo tayari kuanza ujenzi huo wa barabara ambao una urefu wa kilometa kumi na mbili nukta moja sita .
Hata hivyo ametoa shukrani zake kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha ya utekelezaji wa miradi katika baadhi ya miradi katika kata ya hiyo.
Amesema tayari mpaka hivi sasa darasa moja katika shule ya msingi msamadi iliyopo kijiji cha kwasadala umekamilika na ukarabati mwingine unaendelea shuleni apo.
Mhe Pangani amesema njia pekee ya kutunza rasilimali za nchi ni pamoja na kumshirikisha mwananchi kwa kila chanzo kipya cha maendeleo ili awe balozi bora katika miradi inayotekelezwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai