Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imewataka wananchi kushiriki kwenye miradi ya maendeleo inayoendelea ili kujua thamani ya miradi hiyo kwani ni miradi inayoletwa Kwa ajili Yao.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo Septemba 28 2022 Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Said Irando amesema kuwa viongozi wanaosimamia miradi ya maendeleo kwenye ngazi ya Vijiji, Vitongoji, kata na wilaya kuhakikisha wananchi wanashirikishwa na kujua thamani ya miradi hiyo.
“Niwashukuru wazazi Kwa hatua ya kushirikiana na serikali Kwa ajili ya manufaa ya watoto wanaosoma hapa na watakaokuja kujiunga kusoma katika madarasa haya, viongozi hakikisheni mnawashirikisha hawa wananchi kwasababu miradi inayoletwa na Mhe. Rais ni kwa ajili ya wananchi, nawapongeza sana endeleeni na ushirikiano huo huo”Mhe. Irando
Aidha Irando amewataka waliopewa kazi ya kuisimamia miradi hiyo kuhakikisha wanaisimamia na kuikamilisha kwa wakati kwani mradi unapochukua mda mrefu huleta hasara kutokana na kubadilika kwa gharama na vifaa vya ujenzi kila mara.
Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wella amesema ni utaratibu wa kamati ya ulinzi na usalama kutembelea miradi hiyo lengo ni kuona yanayoendelea na si kuishia kupokea taarifa huku akiwataka wananchi kuiunga mkono serikali ya Rais Samia Suluh Hassani kwa kushiriki kazi zinazokuwa zikiendelea kwenye miradi hiyo.
“Imekuwa kawaida yetu sisi Kama kamati ya ulinzi na usalama kutembelea na kukagua miradi ya mandeleo katika wilaya yetu lakini katika maeneo tuliyopita kukagua ujenzi unaendelea kwa hatua nzuri, rai yangu kwa wananchi kushiriki kuiunga mkono serikali kwa kazi ambazo zinafanywa kwani serikali haiwezi kufanya kazi peke yake” Upendo Wella
Baadhi ya miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na Ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu sita ya vyoo shule ya msingi Kikavu chini ambao upo kwenye hatua ya umaliziaji,ujenzi wa nyumba za walimu(two in one),ujenzi wa darasa moja ambalo linatokana na nguvu za wananchi ambapo pia serikali iliunga mkono umaliziaji wa ujenzi huo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai