Mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amewataka wananchi wa kata ya Narumu wanaoishi katika mikoa mingine kushirikiana na serekali kufanyia ukarabati shule ya msingi Orori .
Saashisha ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika kata ya Narumu na kufika katika shule ya hiyo ambapo alikabidhi mifuko ya saruji thelathini pamoja na mabati ishirini na tano kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na mbili.
Saashisha amesema kuwa tayari serikali imetoa fedha kupitia mradi wa EP4R ambao umejenga darasa la awali hivyo ni wakati wa wananchi wa kata hiyo kushirikiana na serekali katika shughuli za maendeleo badala ya kuiachia serekali kufanya kila kitu.
“nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wa kata ya Narumu wanaoishi Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na mikoa mingine mingi waone umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo , wapo watu waliosoma hapa na kwa sasa Mungu amewabariki naomba mrudishe kitu hapa, njooni tulete maendeleo nyumbani, huu ni wajibu wetu, tuibadilishe shule hii.”amesisitiza Saashisha Mafuwe.
Awali mkuu wa shule hiyo ndugu Zubeda Mayange akisoma taarifa ya shule hiyo amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali hasa uhaba wa matundu ya vyoo ambayo Mafue tayari ametoa mifuko 30 ya saruji na mabati 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu hayo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Narumu ndugu John Lengai amemshukuru mbunge kwa kufika katika kata hiyo na kutoa mchango wa saruji na mabati kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo .
“kwa kweli nimshukuru Mh mbunge kwa niaba ya wananchi wa kata ya narumu,kwanza kwa kufika na kukabidhi vifaa hivi,lakini pia nimuhaidi kuwa yale yote aliyoyaagiza nitakwenda kuyatekeleza kwa ajili ya maslajhi ya kata hii.” John Lengai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai