Kufuatia kuwepo kwa fedha za bandia, mkuu wawilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya ametoa siku tatu za msamaha kwa wananchi wote waliopokea fedha hizo bila kujua kuzisalimisha ofisini kwake au kituo cha polisi hadi ifikapo ijumaa ya tarehe 25 octoba mwaka huu.
Pamoja na kutoa siku hizo tatu pia amewatoa hofu wananchi wenye fedha hizo kuwa pindi watakapozisalimisha ofisini kwake au kwa mkuu wa polisi Hai hawatachukuliwa hatua yoyote ya kisheria kama ilivyo hofu mionngoni mwao.
Ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wafanya biashara pamoja na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya stend ya mabasi Bomang’ombe ambao pia ulibeba lengo lakutoa elimu ya utambuzi wa alama za usalama na utunzaji bora wa noti pamoja na utambuzi wa fedha bandia elimu iliyotolewa na wataalamu kutoka benki kuu Tanzania tawi la Arusha.
Amesema “natoa msamaha huu kwakuwa hamkuwa na elimu ya kutambua fedha bandia,baada ya siku hizi tatu kuisha kwakuwa tumeshatoa elimu mtu yoyote tutakaye mkamata atakchuliwa hatua za kisheria na msamaha huu hatuawahusu wale mawakala wanatengeneza na kusambaza fedha hizi za bandia ”.
Sabaya amesema kuwa uwepo wa fedha hizo ndani ya jamii kunaleta athari kubwa ikiwemo kusababisha mfumuko wa bei na mzunguko usio wa uhalisia kutokana na fedha hizo kutokuwa halali, hivyo wameona ni vyema kuwaalika maafisa hao ili kutoa elimu ya utambuzi wa fedha hizo kwa wafanya biasha na wananchi itakayowasaidi kufahamu uhalisia wa fedha halali na bandia.
Aidha baada ya kupata elimu hiyo amewataka wananchi kuwa makini wanapofanya biashara zao ili kuepukana na tatizo hilo la kupatiwa fedha bandia.
Kwa upande wake meneja msaidizi kitengo cha sarafu Banki kuu tawi la Arusha Bw.Robert Methew amesema kuwa baada ya kupata ombi kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya waliona ni vema kufika na kutoa elimu hiyo kwa wananchi ili kupata utambuzi wa noti halali hivyo amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza fedha na wanapogundua ni bandia watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama ili hatua stahiki zichukuliwe.
Hivi karibuni kamati ya ulinzi na usalama wilayani Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo iliweka mtego na kufanikisha kumkamata Richard Mtui aikiwa na noti bandia yenye thamani ya shilingi milioni 11ambazo alilenga kuzisambaza katika wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai