Wanufaika wa TASAF Hai Waishukuru Serikali Kuwathamini
Imetumwa: March 17th, 2021
WANUFAIKA wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kiuchumi kupitia ruzuku wanayopokea, hali iliyowaondolea umaskini uliokithiri katika kaya zao kutokana na kuwa na uhakika wa kuendesha maisha yao na ya familia zao.
Pia wamewashauri wanufaika wengine kuweka akiba, ili ruzuku hiyo iwaondoe kwenye umaskini kama serikali ilivyodhamiria.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Kijiji Cha Kwasadala Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wakati wakipokea fedha hizo leo ,wanufaika hao wa TASAF walisema awali kabla ya kuingizwa katika mpango huo, walikuwa na maisha magumu kutokana na kuishi katika nyumba za tende huku hali ya lishe na elimu kwa watoto ikiwa ni shida.
Bi.Munieshi Mose ambaye ni mnufaika wamuda Mrefu amekiri kuwa TASAF, imemtoa katika umaskini baada ya kuanza ufugaji wa mifugo mbalimbali pamoja na kuku baada ya kuanza kupokea fedha za ruzuku kutoka katika mfuko huo, ambapo sasa inamuwezesha kupata mahitaji yafamilia ikiwa nipamoja na kumuuguza mine wake ambae ni mgonjwa.
Mkazi mwingine wa Kitongoji cha Matowo Kijiji Cha Kwasadala Nuru Seifu Mtela ameiomba serikali kuangalia uwezekano wakuwaongezea kiwango Cha fedha hasa kwa wale wanaopokea kiwango Cha chini kinachoanzia shilingi elfu 10 Hadi elfu 20 alisema kuwa itawasaidia zaidi kuinuka kiuchumi.
Amesema"tunatoa shukurani kwaserikali yetu kwakuweza kutusaidia lakini tuko tofauti,Kuna ambao wanasaidiwa kukifungu chachini na wengine kifungu Cha juu,kwamfano sisi elfu 10 Hadi 20,hiyo nayo serikali yetu ingetuangalia ikatuongezea hapo ata kidogo kwasababu Shilingi elfu 10 au 20 unakwenda nayo sasa ukienda nayo usipokuwa na busara utajikuta Kila siku tu unakwenda nakurudi hivihivi,kweli serikali imetutizama vizuri sasa naiomba uwatazame wale wa chini".
Pia amewashahuri wanufaika wengine wajitahidi kuweka akiba, ili wafanye mambo ya maana ili hata mradi utakapoisha wawe na miradi endelevu itakayowasaidia wao na jamii inayowazunguka.
Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Hai Bw. Michael Mumburi amesema kuwa TASAF Wilaya ya Hai mpaka sasa imefanikiwa kuzifikia Kaya 3,533 katika kipindi Cha malipo ya mwezi Novemba na Disemba 2020 ambapo imepokea kiasi Cha Shilingi milioni 185,131,870