Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amewataka wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuwa waangalifu na kusimamia vema fedha zinazotolewa na serikali ili kukamalisha miradi hiyo kwa wakati.
Amebainisha hayo wakati akitembelea miradi ya maendeleo katika wilaya ya Hai ikiwemo shule ya msingi Mlima Shabaha, shule ya msingi Kingereka, shule ya sekondari Harambee, shule ya sekondari ya Machame girls, kituo cha afya cha Kisiki pamoja na ujenzi wa barabara ya Snow view.
Hata hivyo amewaomba wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo Martha Zablon ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambi ya Raha ametoa shukrani za dhati kwa serikali kwa kutoa kiasi cha shilingi 348,500,000.00 ujenzi wa shule hiyo mpya.
Nao wakazi wa eneo hilo wamefurahishwa na ujenzi wa shule hiyo mpya kwani hapo awali wanafunzi walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai