Afisa tawala wilaya ya Hai Mary Mnyawi amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ili wakapatiwe chanjo ya Polio ambayo imeanza kutolewa tena.
Mnyawi amesema hayo wakati akizindua mpango wa chanjo ya Polio mzunguko wa nne itakayofanyika kwa siku nne kuanzia Disemba 01, hadi 04, 2022 ikiwalenga watoto chini ya miaka mitano (5).
“nchi ya Malawi wamepata shida hiyo (polio) lakini Serikali yetu ikaona ni bora kuwahi kinga kuliko kutibu kama tulivyosikia kwamba kutibu ni gharama na ndio maana Serikali iliona kwamba tayari majirani zetu wameshapata athari hii, sasa sisi tuweze kupata chanjo hii mapema”
Mganga mkuu wa wilaya ya Hai Dkt. Itikija Msuya ameeleza kuwa katika kampeni hiyo awamu ya tatu wilaya ilivuka lengo na kufikia asilimia 153% na kuahidi pia katika awamu nne watahakikisha wanatimiza lengo la Serikali la kuchanja watoto wote wanaostahili kupatiwa chanjo hiyo.
“tutapita nyumba baada ya nyumba ili kuhakikisha watoto wote ambao wanastahili kupata chanjo wanapata kwa sababu ni haki yao ya msingi kwa kuwa tusipowapatia chanjo hii sawasawa ni sawa na kuwafanyia ukatili na sisi hatutaki kufanya ukatili kwa watoto hawa”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai