Serikali imetenga shilingi bilioni 3.1 kwa ajili ya kutatua kero ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro tatizo ambalo limekua sugu kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Yohana Sintoo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Sintoo ameyasema hayo wakati akijibu swali la diwani wa viti maalumu upendo sawe alilouliza ni lini serikali itatekeleza kauli ya kumtua mama ndoo kichwani katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya hai yenye changamoto ya muda mrefu.
Nae mwenyekiti wa wilaya ya hai Edmund Lutaraka amewataka watendaji wa kata pamoja na watendaji wa vijiji kuwa pamoja kuhakikisha vijiji vinakua salama kwani fedha nyingi zimetolewa na serikali kwa ajili ya huduma mbali mbali.
Aidha katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na katibu tawala wilaya ya hai Upendo Wela nakuwapongeza madimani kwa ushirikiano pamoja na utulivu tofauti na vikako vingine vinavyo fanyika katika sehemu nyingine.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai