Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imekuwa ya kwanza mkoani humo katika kutekeleza mpango wa kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa mwaka 2019 kwa kutoa kinga tiba asilimia 99.3 ya malengo waliyokuwa wamewekewa na Wizara ya Afya.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya mwaka jana katika kikao cha uandaa mpango mkakati wa mwaka 2020,maratibu wa mango huo Dkt Apolnary Tesha amesema wamefikia kiwango hicho kutokana na ushirikiano wa viongozi wa ngazi mbali mbali pamoja na uhamasishaji uliofanywa kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na redio Boma.
Amesema kwa kipindi cha mwaka 2019 waliwekewa malengo ya kutoa dawa kwa watoto 40,840 na walifanikiwa kutoa dawa kwa watoto 40,595 na kwamba kwa kipindi cha mwaka huu wanatarajia kutoa dawa za minyoo kwa watoto 42,942.
Kufuatia taarifa hiyo ,katibu tawala wa wilaya ya Hai bi Upendo Wella kwa niaba ya Mkuu wa wilaya,ameipongeza idara ya afya kwa kufanikiwa kutoa kinga tiba kwa kiwango hicho na kutaka mwaka 2020 ,kuhakikisha wanatoa kwa asilimia 100 kwakuwa changamoto zilizojitokeza mwaka jana nyingi zinaweza kufanyiwa kazi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai