Wilaya ya Hai imepokea jumla ya shilingi milioni 950 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari, vitakavyojengwa katika kata 13 kati ya kata 17 za wilaya hiyo.
Kutokana na fedha hizo jumla ya shilingi milioni 860 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa pamoja na madawati yake.
Akizungumza na Redio Boma Hai fm ofisini kwake leo, Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella, ameeleza kuwa pamoja na ujenzi huo wa vyumba vya madarasa wametenga jumla ya shilingi milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya ambayo itakuwa na uwezo wa kuishi watumishi watatu wa kada hiyo.
Aidha ameeleza mradi huo, umelenga kutekelezwa katika shule za sekondari kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi watakaochaguliwa mwakani kujiunga na kidato cha kwanza waweze kupata madarasa ya kusomea ikiwa ni pamoja na kupunguza mrundikano wa wanafunzi darasani kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa UVICO-19.
Katibu tawala huyo amewataka wale wote watakaohusika katika utekelezaji wa miradi inayotokana na fedha hizo kuhakikisha wanafanya kazi kulingana na miongozo na vigezo vilivyowekwa, ili kutekeleza kikamilifu mpango huo ambao umeanzishwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Sambamba na hayo Katibu tawala Upendo Wella ametoa rai kwa wananchi na wadau mbalimbali katika ngazi ya vijiji kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli za ujenzi wa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuchimba misingi wakati ambapo miradi hiyo itaanza kutekelezwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai