Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella (katikati mwenye miwani na skafu nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Yohana Sintoo (mrefu aliyevaa suti ya kijivu), Diwani wa Kata ya Masama Magharibi Elibariki Mbise (aliyevaa tracksuit ya buluu), viongozi wa ngazi mbalimbali, watumishi wa umma na wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa kilimo cha zao la Korosho iliyofanyika kwenye jengo la Kituo cha Rasilimali za Kilimo cha Kata (WARC) na baadaye kwenye shamba la Shule ya Msingi Rundugai ambapo miche ya korosho imeoteshwa katika ekari 2 za shamba la shule hiyo litakalotumika kama shamba darasa.
Uzinduzi huo umefanyika mapema tarehe 17/05/2018 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha kilimo cha mazao matano makuu ya biashara ikiwemo korosho iliyothibitishwa na wataalamu wa kilimo kuwa inaweza kustawi kwenye baadhi ya maeneo ya ukanda wa tambarare katika Wilaya ya Hai.
Kilimo cha korosho kinatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi ndani ya wilaya kutokana na mauzo ya zao hilo pale yatakapofikia wakati wa mavuno.