Watumishi wilayani hai wametakiwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliostaafu utumishi wa umma katika idara ya kilimo na mifugo mkurigenzi mtendaji wa wilata ya Hai Yohana Sintoo amesema kuwa siri kubwa ya mafanikio katika idara yeyote ni kuonesha umoja na mshikamano katika utendaji wa kila siku.
Aidha pia Sintoo amechukua nafasi hiyo kuwataka watendaji katika idara hiyo kuendelea kuchapa kazi ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dkt John Magufuli inazidi kutoa fedha nyingi kusaidia sekta ya kilimo hapa nchini.
Awali akizungumza kwa niaba ya wastaafu wenzake Eliya Machange amesema kuwa utumishi wa umma ni dhamana hivyo haina budi kwa wanaobaki kazini kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na taratibu katika utumishi wa umma
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai