SERIKALI wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro imewataka askari wa jeshi la akiba (Mgambo) kuzingatia maadili na nidhamu ya kazi ili kuimarisha ulinzi na usalama na kuwa waadilifu pamoja na kuchunga kiapo cha utii ili watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa wilaya hiyo Juma Irando alitoa kauli hiyo Dec 08, 2021 wakati akifunga mafunzo kwa askari wa jeshi hilo katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru ambapo amewataka kushirikiana na Jamii na kuwa walinzi wa mfano kwa kuwasaidia Wananchi matatizo mbalimbali ya kiusalama zaidi pia wawe wanatoa taarifa za Rushwa bila kusita endapo watabaini kuna vitendo au viashiria.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka kushirikiana na Jamii na kuwa walinzi wa mfano kwa kuwasaidia Wananchi katika matatizo mbalimbali ya kiusalama.
Aliwataka askari hao kuhakikisha mafunzo waliyopata wanatekeleza kwa vitendo na kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii inayowazuka.
“Askari wengine wa jeshi la akiba wakipata mafunzo hayo huonesha ubabe kwa jamii bila sababu ya msingi na tumekuwa tukiletewa malalamiko yao na kesi zao tunazo”
“Idadi ya askari waliopo hawatoshi ndiyo maana serikali yetu ilibuni jeshi hili la akiba ili liweze kuziba mapengo haya badala ya kutengeneza jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na vyombo vingine vya ulinzi katika kulinda usalama wan chi yetu”
Aidha amewataka kutofumbia macho viashiria vyovyote vinavyoonesha dalili ya kukwamisha kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya sita akiwataka kuisaidia halmashauri hiyo katika kuongeza makusanyo ya mapato.
DC Irando alipongeza juhudi za mshauri wa jeshi la akiba katika wilaya hiyo,Meja Gwamaka Ngondya kwa kuwaandaa vijana wanaoshiriki mafunzo hayo ambayo yamewafanya kuwa wakakamavu kiaskari kwa kuilinda nchi yao na kupambana na uhalifu wa aina yoyote katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Awali akisoma risala ya wahitimu hao , Andrew Msuya alisema mafunzo hayo yamekabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama za kuchangia michango mbali mbali inayohusu mafunzo kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Mafunzo hayo ya jeshi la akiba wilayani Hai yalianza rasmi Julai 19 mwaka huu ambapo jumla ya wanafunzi 84 walianza na waliofanikiwa kuhitimu ni 43 kati yao wanaume 35 na wanawake ni 8.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai