Mkuu wa wilaya ya Hai Lazaro Twange amewataka watendaji wa vijiji,Wenyekiti wa Vijiji pamoja na Wenyeviti wa Vitongoji kudhibiti biashara na matumizi ya pombe haramu katika vijiji vyao hali inayosababisha upotevu wa nguvu kazi katika jamii.
Hayo ameyazungumza katika kikao na viongozi hao katika ukumbi wa polisi uliopo wilayani Hai Desemba 19, 2024 na kuwataka viongozi hao kushughulikia biashara hiyo inayopunguza kasi ya maendeleo katika jamii zetu.
Pia amewataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia vyema wananchi kwa kuwasikiliza matatizo yao kuangalia njia za kuweza kuyatatua na kutokujihusisha na matukio mbali mbali yatakayopelekea migogoro katika maeneo yao.
Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Dionis Myinga amewataka Wenyeviti hao,hasa wanaotoka maeneo yaliyopimwa kusimamia sheria ya kutozika mijini.
Myinga amesema kwa kuzika katika maeneo yaliyopimwa si kwamba tu kinyume na sheria lakini pia inapoteza thamani ya ardhi hiyo.
Naye Mkuu wa Divisheni Utawala na Rasilimali watu Hai Barakani Urio amewakumbusha majukumu muhimu ya wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji,changamoto zilizopo katika uendeshaji wa shughuli za kijiji pamoja na namna Halmashauri ilivyojipanga kukabiliana na changamoto mbali mbali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai