Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Hai Dionis Myinga ameshiriki katika Zoezi la Kupiga kura katika kituo cha Bomani ambapo amewashukuru Wananchi wote na kuendelea kutoa wito kuendelea kupiga kura kwa amani na utulivu.
Myinga ameongeza kwa kuwaomba wasimamizi wa uchaguzi kuendelea kusimamia watu wapige kura kwa haraka ili Kuondoa foleni katika vituo vya kupiga kura pamoja na kulinda amani wakati wote wa uchaguzi na hata baada ya Matokeo ya Uchaguzi.
Amesema katika wilaya ya Hai Kuna vijiji 62 na vitongoji 292 ambavyo vyote vinawagombea,vile vile amesema vyama vitatu ndio vimetoa wagombea kuwania nafasi za uongozi ambavyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na ACT Wazalendo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai