Serekali wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imeanza rasmi ujenzi wa madaraja saba ikiwa ni pamoja na kunyanyua tuta za barabara mradi unaotarajiwa kugharimu Zaidi ya bilioni 5.
Akipokea taarifa ya wakala wa barabara katika hafla yakumkabidhi makandarasi eneo la kazi iliyofanyika eneo la Kia wilayani humo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema nia ya Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hasan ni kupunguza vifo vinavyotokana na majanga ya tabia nchi ndio manaa serekali imekuwa ikitumia fadha nyingi katika miradi ya aina hiyo.
Ameongeza kuwa mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa iliyoadhiriwa na mvua za el nino zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu nakutaja eneo la Kia na Kwasomali kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoadhirika na mvua hizo hivyo kuperekea serekali kuja na mpango madhubuti wa kuzuia maafa hayo.
Babu pia amewataka wakandarasi waliokabidhiwa kujumu la ujenzi huo kuakikisha wanafanya kazi kwa weledi na haraka kwa kuzingatia muda waliopewa kwenye mkataba ili wananchi waweze kufaidi matunda ya kuichagua serekali hii.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Hai amesema miradi lukuki inayomiminika katika wilaya ya Hai ni kidhibitisho tosha cha namna mh Rais Dr Samia Suluhu Hasani anavyowapenda watanzania na wato wa Hai kwa ujumla huku akiahidi kuusimamia vyema mradi huo kuanzia mwanzo mpaka mwisho ili uweze kuwanufaisha wananchi
Mradi huu ni matokeo ya fedha zilizotolewa na benki kuu ya dunia kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya madaraja katika maeneo yote yaliyoadhiriwa na mvua nchini ambapo mkataba wa ujenzi wa miundombinu hiyo ulisainiwa tarehe 1 November 2024 kati ya mtendaji mkuu wa wakala wa barabara Tanzania na mkandarasi KINGS BUILDERS LTD na kushuhudiwa na waziri wa ujenzi mh Innosent Bashungwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai