Madereva bodaboda na bajaji wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Barabara hiyo inayojengwa imeelezwa kupunguza hadha kwa wasafiri na wasafirishaji na kuondokana na tatizo la vumbi na ubovu wa barabara.
Richard Gonja ambaye ni dereva bajaji ,akiongea baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu kukagua barabara hiyo amesema uwepo wa barabara kumewasaidia kutarahisisha kazi yao kwani miundombinu imekuwa rafiki na imepunguza kuharibika kwa vifaa vya usafiri.
Naye mfanya biashara wa mahindi katika eneo karibu na baraba hiyo Omary Sila ameishukuru serikali kwa kutengeneza barabara kwani imesaidia wateja wao kufika kwa urahisi na kuzuia vumbi.
Sila amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuijali wilaya ya Hai kwa kuelekeza miradi mingi ya maendeleo wilayani humo.
Pia Shedrack Ndosi mkazi wa Rundugai amesema kuwa ujenzi wa barabara umepunguza adha ya kukwama kwa vyombo vya usafiri wakati wa mvua kwani kwakuwa barabara zimejengewa mitaro ya kupitisha maji taka.
Awali akisoma taarifa kwa mkuu wa Mkoa ,Meneja wa TARURA wilaya ya Hai mhandisi Fuya Francis amesema hadi kukamilika kwa barabara hiyo itajengwa kwa urefu wa km 25.7 kwa gharama ya shilingi bilioni 20.03 ambapo wamu ya kwanza imejengwa mita 500 kwa gharama za milioni 299 na awamu ya pili ya ujenzi inakaribia kuanza.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai