Kamati ya fedha wilaya ya Hai ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi katika shule ya Sekondari Hai Day,shule ya Sekondari Saashisha pamoja na Zahanati ya Kia.
Katika ziara hiyo kamati ya fedha imepokea taarifa ya miradi miwili ya ujenzi wa mabweni manne katika Shule ya Sekondari ya Hai ambapo shule ilipokea kiasi cha fedha shilingi 520,000,000 kupitia miradi ya SEQUIP na EP4R.
Aidha katika ziara hiyo kamati ya fedha ilikagua utekelezaji wa mradi shule ya Sekondari Saashisha iliyopokea kiasi cha fedha 479,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili,madarasa manne,vyoo matundu kumi na nyumba moja ya walimu.
Hata hivyo katika mradi wa shule hiyo madarasa manne yapo katika hatua ya kumwaga jamvi,mabweni ni kujaza vifusi na kumwaga mawe,nyumba ya walimu kumwaga vifusi pamoja na ujenzi wa ukuta wa choo.
Pia kamati ya fedha ilikamilisha ziara yake kwa kutembelea zahanati ya Kia na kupokea taarifa ya mradi wa maji na usafi vijijini ambao utagharimu kiasi cha shilingi 46,000,000 na fedha hiyo ilitolewa na serikali kuu.
Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya kunawa mikono,ukarabati wa choo katika chumba cha kujifungulia,ukarabati wa choo cha wagonjwa,ujenzi wa shimo la kutupia majivu,ujenzi wa shimo la plasenta pamoja ujenzi wa shimo la kuchomea taka,ujenzi wa mnara wa tenki na uwekaji wa tenki la maji.
Miongoni mwa kazi zilizofanyika hadi sasa katika mradi huo ni ujenzi wa sehemu ya kunawa mikono hatua za mwisho,ujenzi wa shimo la kutupia majivu,ujenzi wa mnara wa tenki,ujenzi wa kichomea taka na kazi zinazoendelea ni pamoja na ukarabati wa choo cha wagonjwa vyumba viwili kwa jinsia ya kike pamoja na jinsia ya kiume.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai