Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Wilaya ya Hai imewataka Madiwani kusimamia kikamilifu fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali kwaajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha hizo inaoneka.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani, kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Hai, Josiah Gunda alisema kuwa endapo madiwani watasimamia vizuri fedha za maendeleo itasaidia kupata miradi ilio bora na yenye thamani halisi.
"Fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi madarasa, vituo vya afya, miundombinu ya barabara pamoja na miradi mingine ya maendeleo naomba mkasimamie kikamilifu usiku na mchana ili thamani ya fedha hizo Ikaonekane," alisema Gunda.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai