Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini na mijini (RUWASA) wametakiwa kutoa bei elekezi ya maji kwa wananchi.
Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai. Ndg. Wang’uba Maganda wakati wa ziara ya kamati ya chama hicho kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye ujenzi wa tanki la maji lenye urefu wa mita sita uliopo eneo la Kimambogo kata ya Bondeni.
Mwenyekiti aliwataka wakala hao kutoa bei elekezi kwa wananchi kwakuwa wananchi wengi hawana uelewa sahihi wa kiwango wanachostahili kulipa baada ya kupata hudmuam hiyo muhimu.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja wa RUWASA wilaya ya Hai Emmanuel Mwampashi amesema tanki hilo lilianza kujengwa Mwezi Disemba 2022 kwa gharama ya Shillingi 100,000,000.
Amesema tanki hilo lina ukubwa wa mita za ujazo 100 sawa na lita (100,000), linatumia chanzo kikuu cha maji cha chem chem ya Musa Toroka chenye uwezo wa kuzalisha lita 120 kwa sekunde kilichopo Rundugai Kata Ya Masama Rundugai.
Amesema maji hayo yanatarajiwa kusaidia wakazi zaidi ya 9,500 kutoka vijiji vya kawaya, Rundugai, na Cheki Maji.
Kwa upande mwingine Mwampashi amewataka wananchi kuendelea kulinda vyanzo vya maji pamoja na miundo mbinu iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ili iweze ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kutoa huduma muhimu kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
Mradi unatekelezwa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Maji wa Taifa, unaofanywa na wataalamu wa ndani, na kusimamiwa na ‘RUWASA’ Wilaya, Mkoa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai